Nikiwa kama mdau wa taaluma ya fundi sanifu viungo bandia napata tafsiri kwamba.
Kwa sasa nchi yetu ina wataalam husika wa kutosheleza jamii yote ya watanzania.Tafsiri hii inatokana na nafasi za mafunzo katika tangazo husika fani ya Fundi sanifu viungo bandia (Prosthetist/Orthotist/Orthopaedic Technologist) haipo.
Lakini kwa uzoefu wangu ni kwamba bado watanzania wanaendelea kutumia gharama nyingi kufuata huduma za viungo bandia katika vituo vilivyopo Dar es salaam( Taasisi ya mifupa MOI) ,KCMC Moshi na CCBRT ambavyo ndiko huduma hizi ni za uhakika.
Hivyo changamoto ambayo wizara ya afya inayo ni kuandaa wataalam hawa na kuwawekea miundombinu ya kuwawezesha kusaidia wenye mahitaji katika mikoa yote.
Tanzania baada ya miaka 48 ya uhuru si halali mlemavu anatoka Kigoma,Tabora,Mbeya nk. kufuata huduma ktk vituo nilivyotaja.
No comments:
Post a Comment